Nchi 5 zinamiliki zaidi ya nusu ya uchumi wa dunia
Akinukuu taarifa za kiuchumi za benki ya dunia na IMF wanauchumi wa mtandao wa sualcapitalist.com, Avery Koop, anazitaja nchi hizo kuwa ni Marekani, China, Japan, Ujerumani na India zinazomiliki asilimia 51 ya pato la dunia.
Ukiongeza nchi nyingine 5 na hivyo na nchi 10 bora, mataifa hayo 10 yanamiliki asilimia 66 ya uchumi wa dunia. Mataifa yanayoongezeka hapa ni Uingerea, Ufaransa, Canada, Urusi na Italia.
Yakiongezeka mataifa 15 na kufanya mataifa makubwa kuwa 25, haya yanamiliki asilimia 84 ya uchumi wa dunia na kuyaacha takribani mataifa 165 yakimiliki asilimia 16 tu ya uchumi wa dunia. Mataifa 15 yanayoongezeka na kufanya mataifa 25 ni Iran, Brazil, Korea Kusini, Australia, Mexico, Hispania, Indonesia, Suadi Arabia, Uholanzi, Uturuki, Taiwan, Uswis, Poland, Argentina, Sweden, Ubelgiji, Thailand, Israel, Ireland na Norway.