Thursday 10 November 2016

TRUMP Rais Mpya wa Marekani


Jana, Novemba 9, 2016, Bilionea Donald Trump wa chama cha Republican alifanikiwa kushinda uchaguzi na kuwa Rais wa 45 wa taifa kubwa duniani la Marekani, akimshinda Hillary Clinton kwa kura za wajumbe (Electoral Votes) 276 kwa 218.

Donald Trump, kwa mujibu wa Katiba ya Marekani anatarajiwa kuapishwa rasmi Januari 20, 2017 na kumrithi Baraka Obama wa Chama cha Democrat.

Thursday 11 August 2016

MATOKEO YA DARASA LA NNE 2015


Kwa mara ya kwanza, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa matokeo ya darasa la nne na kuonekana waziwazi kwenye tovuti. Mzazi au mlezi akitaka jina la mtoto wake analipata kwa urahisi zaidi. Hii ni hatua bora kabisa katika upashanaji wa habari, hasa habari muhimu kwa wananchi unaofanywa na serikali yetu. Hii inaondoa pia udanganyifu ambao wazazi wasiokuwa na elimu wamekuwa wakiupata kwa watoto wao kuwadanganya matokeo.

HAYA NDIYO MATOKEO YA DARASA LA NNE 2015. BONYEZA HAPAPermalink
 KUYAONA

MATOKEO YA DARASA LA NNE na SABA 2015


Kwa mara ya kwanza, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa matokeo ya darasa la nne na kuonekana waziwazi kwenye tovuti. Mzazi au mlezi akitaka jina la mtoto wake analipata kwa urahisi zaidi. Hii ni hatua bora kabisa katika upashanaji wa habari, hasa habari muhimu kwa wananchi unaofanywa na serikali yetu. Hii inaondoa pia udanganyifu ambao wazazi wasiokuwa na elimu wamekuwa wakiupata kwa watoto wao kuwadanganya matokeo. Pia matokeo ya darasa la SABA yalitangazwa kwa mtindo uleule pamoja na kwamba siyo mara ya kwanza kufanya hivyo. Naipongeza Wizara ya Elimu kwa kutambua umuhimu wa mtandao katika kuwasiliana na wananchi

HAYA NDIYO MATOKEO YA DARASA LA NNE 2015. BONYEZA HAPA KUONA MATOKEO YA DARASA LA NNE. NA BONYEZA HAPA KUONA MATOKEO YA DARASA LA SABA

Saturday 16 July 2016

Friday 1 July 2016

MKUTANO WA BUNGE LA KUMI NA MOJA WAAHIRISHWA

Mkutano wa 3 wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania uliahirishwa Juni 30, 2016. Akizungumza katika hitimisho hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizitaka Halmashauri zote nchini kutumia mashine za elektroniki katika kukusanya mapato katika mwaka wa fedha unaoanza Julai mosi 2016.


TANZANIA YAPATA WAKUU WAPYA WA WILAYA

Juni 26, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliteua wakuu wa wilaya watakaosaidia katika kulisukuma gurudumu la maendeleo katika uongozi wa awamu ya tano. BONYA HAPA kupata majina ya wakuu wa wilaya.


Tuesday 14 June 2016

NampendaNitamlinda: African Child's Day, June 16 2016







For more information, visit Tanzania Media Women's Association (TAMWA)  social media campaign #NampendaNitamlinda



Thursday 9 June 2016

BAJETI 2016/2017 YATANGAZWA

Jana Juni 8, 2016, Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Philip Isdor Mpango, alisoma bajeti ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2016/2017 ambayo imeonyesha kuweka kipaumbele kwenye kukuza sekta ya viwanda. Bovya maandishi ya herufi kubwa kusoma bajeti nzima kutoka tovuti ya serikali: BAJETI YA TANZANIA 2016/2017

Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Pius Mpango


Tuesday 7 June 2016

Nampenda Nitamlinda

Credit: TAMWA campaign on ‪#‎NAMPENDANITAMLINDA‬ ‪#‎TAMWA‬

Nampenda Nitamlinda

Credit: TAMWA campaign on ‪#‎NAMPENDANITAMLINDA‬ ‪#‎TAMWA‬